Jumanne 23 Desemba 2025 - 16:30
Njia ya mapambano ya muqawa.a ndiyo chaguo lenye mafanikio zaidi

Hawza/ Kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa tisa tangia kufariki Sheikh Abdulnaser Jabri, Harakati ya Umma wa Lebanon (Harakat al-Ummah) iliandaa kikao cha kielimu na kisiasa kwenye makao makuu ya harakati hiyo, kwa ushiriki wa idadi ya watu mashuhuri wa kielimu na kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika maadhimisho ya mwaka wa tisa wa kifo cha Sheikh Abdulnaser Jabri, Harakati ya Umma wa Lebanon iliandaa kikao cha kielimu na kisiasa chini ya kaulimbiu “Tunabaki waaminifu kwa ahadi yetu”, katika makao makuu ya harakati hiyo, huku kikihudhuriwa na kundi la shakhsia za kielimu na kisiasa.

Balozi wa Iran: Urithi wa umoja na muqawama wa Sheikh Jabri bado unaendelea kuishi

Mujtaba Amani, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, katika hafla hiyo, alizungumza katika mahojiano na tovuti ya habari ya Al-Ahed kwamba kushiriki katika kumbukumbu ya Sheikh Abdulnaser Jabri ni msisitizo wa kuendelezwa kwa njia ya mtu huyu mkubwa.

Alibainisha kuwa njia ya Sheikh Jabri bado iko hai, na kwamba misingi ya fikra zake pamoja na watoto wake wanaendelea kushikilia mkabala wake wa kuhimiza umoja na mapambano ya muqawama, huku akielezea kuondoka kwake kuwa ni hasara kubwa kwa Umma wa Kiislamu.

Balozi wa Iran pia, katika sehemu ya hotuba yake kwenye kikao hicho alisisitiza kwamba; chaguo la muqawama, katika wakati wowote, ndilo chaguo lenye mafanikio makubwa zaidi, na akabainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama daima bega kwa bega na serikali pamoja na harakati za muqawama.

Sheikh Hassan Abdullah: Kuhamisha utamaduni wa Palestina kwa vizazi vijavyo

Sheikh Hassan Abdullah, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu Lebanon, alisisitiza umuhimu wa kulikabidhi suala la Palestina kwenye vizazi vijavyo, akisema: “Hata kama hatutaweza kuikomboa Palestina, ni lazima tuurithishe utamaduni huu kwa vizazi vinavyokuja.” Aidha, alikumbusha baadhi ya kumbukumbu na matukio yanayomhusu Sheikh Abdulnaser Jabri.

Sheikh Abdullah Jabri: Wito wa kupambana na mradi wa “Israel Kubwa”

Sheikh Abdullah Jabri, Katibu Mkuu wa Harakati ya Umma wa Lebanon, aliwahimiza wapigania uhuru wa Syria kukataa miradi inayotekelezwa katika ardhi yao, na akasisitiza kwamba adui ameanza kwa uwazi kabisa kutekeleza mradi wake wa kuanzisha “Israel Kubwa”, na kwamba Syria ni sehemu ya mradi huo unaopaswa kupingwa na kupigwa vita.

Sheikh Zuhair Jaeed: Ushindi hauwezekani bila ya umoja wa Kiislamu

Sheikh Zuhair Jaeed, Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Utekelezaji wa Kiislamu la Lebanon, alisisitizia umuhimu wa umoja wa Kiislamu katika kukabiliana na changamoto za sasa, akisema: “Mzigo wa muqawama hauwezi kubebwa na Mashia pekee wala na Masunni pekee. Ni lazima tuungane, kwa sababu hatari inaukumba Uislamu kwa ujumla wake, na kwa pamoja hatutashindwa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha